Excel

Learn & Belong

International Center

Home  :  International  :  Welcome  

Karibuni

Chuo cha Parkland hukaribisha wanafunzi wanaotoka katika tamaduni mbali mbali za ulimwengu mzima, katika chuo chetu kila mwaka. Mataifa zaidi ya hamsini huwakilishwa na wanafunzi zaidi ya mia tatu na hamsini, wanaohudhuria chuo cha Parkland. Wengi wao huusika katika vitenzi na vikundi mbali mbali, wakiendelea na vikuu vyao.

Mbona Uchague Chuo Cha Parkland?

Parkland ni mojawapo ya vyuo vinavyoongoza katika jimbo la Illinois, na zaidi ya hati na shahada mia moja hamsini zinazohawili. Inao wafanyanikazi katika ofisi ya wanafunzi wa kimataifa waliojawa na haiba wanaoweza kukupa usaidizi katika utaratibu wa kujiunga na shule, kupa mawaidha kuhusu kingereza ikiwa lugha ya pili na pia, mahitaji zozote mbali mbali za kibinafsi. Chuo cha Parkland itakupa nafasi ya kujiendeleza kimaisha kama mwanafunzi na ukamilishaji wa miradi yako maishani.

Faida Za Kuhudhuria Chuo Cha Parkland:

-- Vikundi vidogo katika madarasa ili kila mwanafunzi apate nafasa ya kuongea na mwalimu.

--Chaguo la darasa zilizoko kupitia mtandao wa internet.

--Vituo vya kuelimishana vinavyosaidia katika masomo mbali mbali kama vile hesabu, na kunadika na kadhalika.

--Zaidi ya vikundi arobaini, vilovyoandikishwa; Kikundi Cha Wanafunzi wa Kimataifa husaidia wanafunzi wa kimataifa kupata marafiki kutoka nchi tofauti tofauti zilizoko ulimweguni, na kuwasaidi kuzoea maisha ya kuwa mwanafunzi huku Amerika.

--Unapewa usaidizi na mawaidha katika uchaguzi wa vikuu mbali mbali

--Tamaduni mbali mbali katika usalama wa mji mdogo

Maelezo Zaidi:

Jamuiya
Chuo Cha Parkland liko  katika mji ilioko magharibi ya kati (Watu Elfu mia moja na hamsini), masaa matatu kutoka jiji la Chicago na Jiji la St.Louis. Ni jirani ya Chuo Kikuu Cha Illinois. Parkland huusika na vitenzi mbali mbali vya elimu na utafiti  ya jumuiya vya kimataifa.

Gharama
Gharama ya elimu katika Chuo cha Parkland ni ya chini, ukilinganisha na vyuo vikuu vingine katika nchi ya America. Ikiwa mumeo ama mkeo ameandikwa kazi katika Wilaya ya 505,unaweza kupewa uwezo wa kulipa ada sawa na mtu anayeishi katika Wilaya ya 505.

Mahitaji Ya Lugha
Hakuna mapato ya kijumla ya TOEFL inayotakikana kuingia katika Programu ya Kiingereza kama Lugha ya Pili. Bofya Mahali Pa ili ujifunze zaidi kuhusu mahitaji ya lugha.

Kuhawili
Chuo Cha Parkland huwapa wanafunzi kozi zinazotakikana kuhawilia katika Chuo Kikuu Cha Illinois. Chuo Kikuu Cha Illinois huwepusha mahitaji ya TOEFL kwa wanafunzi waliohudhuria Chuo cha Parkland kwa Miula minne, na kuchukua zaidi ya masaa kumi na miwili kwa kila muula kabla ya kuhawili.

Did You Know?

Parkland's adult and continuing education program offers credit and noncredit courses that meet the needs of special populations within our district, such as teachers, businesspersons, retirees, and K-12 students.

 
 

© Parkland College
2400 West Bradley Ave | Champaign, IL 61821 | 217.351.2200 | 888.467.6065
The Mission of Parkland College is to engage the community in learning.